Wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) wanazidi kubobea katika taaluma za Qur’an Tukufu na kuandaliwa kuwa wahudumu bora wa Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi

18 Septemba 2025 - 21:24

Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania, Dkt. Ali Taqavi, akifuatilia kwa karibu zaidi maendeleo ya Wanafunzi katika Sayansi za Qur’an Tukufu +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania aliwahimiza na kuwausia wanafunzi kuzingatia Qur’an Tukufu katika masomo yao na katika maisha yao ya kila siku. Alisisitiza kwa kusema: “Qur’an Tukufu ni uhai wetu, na hatakhasirika yeyote atakayeshikamana nayo.”

Kupitia Chuo hiki cha Kisayansi cha Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania, Wanafunzi wanapewa malezi ya kielimu na kiroho katika nyanja mbalimbali za Sayansi za Qur’an Tukufu. Miongoni mwa masomo yanayopewa kipaumbele ni:

1_ Usomaji wa Qur’an na Tajwid sahihi.

2_ Kuhifadhi Qur’an Tukufu.

3_ Tafsiri na ufahamu wa maana na makusudio ya Aya.

4_Tadaburi katika Aya za Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya kuelewa zaidi hekima na mafunzo yake.

Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania, Dkt. Ali Taqavi, akifuatilia kwa karibu zaidi maendeleo ya Wanafunzi katika Sayansi za Qur’an Tukufu +Picha

Kwa njia hii, wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) wanazidi kubobea katika taaluma za Qur’an Tukufu na kuandaliwa kuwa wahudumu bora wa Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha